Friday 15 May 2015

DONDOO ZA KUSHANGAZA TUNAPOSHEREHEKEA SIKUKUU YA MT. ISIDORI MKULIMA NA FIVE SAINTS

 Leo ni sikukuu ya Mt. Isdori Mkulima. Mtakatifu huyu alikuwa ni mlei tu tena mwenye familia yake kutoka Madrid Hispania lakini aliishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Alitangazwa Mt. Tarehe 23 March 1622 na Papa Gregory XV.

Siku hiyo hiyo walitangazwa watakatifu wengine ambao ni



Mt. Isidori Mkulima



Mt. Ignas wa Loyola - Hispania

Teresa wa Avila


Mt.Philip Neri

Mt.Francis Ksaveri


Sikujua kwamba watakatifu hawa wakubwa na maarufu walitangazwa watakatifu siku moja. Lakini Pia kilichonifanya nishangae ni kwamba Mt. Philipo alitaka kujiunga shirika la WAJEZUIT ambalo lilikuwa limeanzishwa na Mt. Ignas wa Loyola na ni kipindi hicho, Francis Ksaveri na Ignas wa Loyola walikuwa ni marafiki wakubwa. Alitamani sana kujiunga na shirika hili ili aende kuwa mmisionari huko India kama alivyofanya Francis Ksaveri lakini kwa mapenzi ya Mungu aliambiwa abaki Roma na kuwa ni mtume wa Roma.

Mt. Isdori mkulima alikuwa ni mkulima lakini aliipenda kazi yake na kumtafakari Mungu katika ukulima wake. Mara nyingi alichelewa kazini kwakuwa alipitia kanisani. Hata hivyo, Malaika walimsaidia katika kazi zake na hasa alipokuwa amechelewa kutoka kanisani au alipokuwa amechoka.

I just wanted to share this story with you friends.

Basi tuwaombe watakatifu hawa na hasa Mt. Isdori Mkulima watuombee kwa Mungu


Katika upendo wa Kristu,

Vincenzia- Marie!

No comments:

Post a Comment