Friday 15 May 2015

CARDINAL TAGLE AWA RAIS MPYA WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA CARITAS

Kardinali Tagle ni kardinali kutoka Ufilipino na anawapenda sana vijana na hasa kutoka katika kikundi chetu cha International Observatory of Young Catholics for Social Justice (IOYCS). Miezi kadhaa iliyopita alitualika kumtembelea nyumbani kwake Manila na kwamba angetukaribisha chai na cookies. Hahhaahahahaha ni mcheshi sana. HONGERA SANA BABA!

Caritas -maana yake Upendo, ni shirika la kanisa katoliki linalosaidia maskini, watu waliotengwa na watu wenye matatizo bila kujali imani ya mtu, wala utaifa. Pia linashunghulikia kukuza upendo na haki duniani.


Kardinai Tagle na Papa Francis


Vijana wa IOYC -Afrika wanapenda kumtakia Kardinali Tagle nguvu na upendo katika kuliongoza shirika hili la kikatoliki duniani.


Katika Upendo wa Kristu,

Vincenzia- Marie, IOYC - Africa!

No comments:

Post a Comment