Wakati nchi ya Kenya inajiandaa na shmra shara za kutangazwa Mwenyeheri kwa Sr. Irene Stefani, Tanzania na nchi zingine za Afrika ya Mashariki yapasa pia tuone fahari hiyo. Wakati wa Vita ya kwanza ya dunia alihudumia wapiganaji walioumia vitani na inasemekana wengine walikuwa nai askari wa Kitanzania.
|
Sr. Irene Stefani |
LAKINI, SR. IRENE STEFANI AU NYAATHA NI NANI HASA?
Sr. Irene, mama wa huruma na upendo alizaliwa nchini Italia Tarehe
22, Agosti mwaka 1891 na alifariki nchini Kenya, Octoba 31 ya mwaka 1930.Mama
wa mapendo na huruma ni sentensi inayojumuisha maisha ya Sr. Irene, maisha ya
kujitoa kwa Mungu kwa ukarimu katika
huduma na uinjilishaji.
Mwaka 1911, akiwa na umri wa miaka 20, Irene aliamua kuwa
mmisionari wa shirika la Consolata, lililokuwa limeanzishwa huko Turin Italia
na Mwenyeheri Joseph Allamano mwaka mmoja nyuma. Januari 29, mwaka 1914, Sr. Irene aliweka nadhiri zake huko Turin
alielezea programu yake ya maisha katika sentesi fupi akisema;
"Ni Yesu pekee, Kabisa
na Yesu, kuwa mali ya Yesu kabisa, Kabisa kwa ajili ya Yesu, fanya haya na
utaishi"
Sista Irene alifika Kenya Januari 1915 na huko aliishi maisha ya
waanzilishi wa kwanza, yaani; katika umaskini mkubwa, kazi ngumu na kutengwa.
Moyo wake wa ukarimu haukujua mipaka ya kujitoa mwenyewe kwa
mapendo makubwa na huruma akiwatangazia wote lulu zake kubwa amnao ni Habari
njema kwamba Yesu, mwana wa Mungu, alikuwa ni mkombozi wao.
|
Mama wa Upendo na Huruma | | |
|
|
Miezi michache baada ya kufika Kenya, Vita vya kwanza vya dunia
ndio vilikuwa vimefika katika makoloni ya Kijerumani na ya Kiingereza huko Afrika
ya Mashariki.
Sr. Irene aliomba kujitolea katika shirika la Msalaba mwekundu
ambao walikuwa wamejikita katika kazi ngumu za huruma kama vile, kuwahudumia
waliumia katika hospitali za jeshi ambazo zilikuwa zimefurika wagonjwa wengi
hasa wale walioumia.
Kwa muda wa miaka mitatu, Sr. Irene alijitoa kishujaa kuwahudumia
kwa upendo na huruma watu waliolazimishwa kwenda vitani na kutelekezwa kufa
baada ya kuumia.
Baada ya vita, Sr. Irene alirudi kwa wapendwa wake wakikuyu ambao
walikuwa wamejizamisha katika kazi ya uinjilishaji, unesi, ualimu a kutembelea
familia kila mara wakiwa tayari kusaidia, kutia moyo, kuongoza kwa upole vijana
ili waweze kuishi imani yao ipasavyo. Kila mahali alifanya kazi kikarimu mno
hadi watu wakamuita "Nyaatha" maana yake "Mama mwenye
huruma"
Mwaka 1930 ulikuwa mgumu katika shirika lao
jipya na kwenye Missioni. Sr. Irene aliyatambua haya yote hivyo aliwaomba wakuu
wake aweze kujitolea maisha yake maskini kwaajili ya Misheni. " Siwezi kusema
hapana - alisema mama Mkuu wa Shirika, mama Ferdinanda, lakini wacha tuyafanye
mapenzi ya Mungu, hakuna zaidi ya kufanya mapenzi ya Mungu"
Sr. Irene alikuwa amepewa ruhusa kubwa ila
hakujua kwamba Mungu angejibu haraka namna ile na kumchukua. yaani, wiki mbili
tu baadae, Sr. Irene aliaga dunia/ alifariki. Alikufa kutokana na ushujaa wake
wa upendo, kwa ugonjwa wa mlipuko uliotokea katika kijiji kimoja naye akaenda
kuhudumia.
Hii ilikuwa ni Octoba ya mwaka 1930.
|
Masalia ya mwili wa Sr. Irene |
Juu na chini ya vilima vya Kikuyu, habari
zilipokelewa kwa maombolezo makubwa ambayo hayakuwahi kutokea kwamba Nyaatha-
mama wa upendo na huruma, alikuwa amewatoka. Mabaki ya mwili wake sasa yapo
katika Kanisa la Consolata, Nyeri huko Kenya. Hata baada ya miaka 50 ya kifo
chake, kumbukumbu zake bado zingali
zinaishi katika mioyo ya watu.
Hata leo, Bado Sr. Irene Nyeri anaendeleza
umisionari wake wa upendo na huruma.
Basi akiwa anatangazwa Mwenyeheri hapo Kesho,
Sherehe zitakazoongozwa na Mwadhama John Kardinali Njue Askofu mkuu wa Nairobi
na hati ya uenyeheri itasomwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Askofu mkuu
wa Dar es Salaam -Tanzania, Wana Afrika ya Mashariki, yapaswa tuione sherehe
yetu hii kama ni yetu sote na tumuombe maombezi yake ili amani itawale katika
nchi zetu.
|
Mwadhama Polycarp Kardinali. Pengo |
|
Watu mbalimbali wakitembelea mahali amabapo Masalia ya Sr. Irene yamewekwa. |
Mojawapo ya miujiza ambayo imefanikisha
kutangazwa mwenye heri ni kipindi cha ukoloni kule Msumbiji ambapo makatekista
na watu waliokimbilia kanisani kutengwa huko bila msaada wowote na hakukuwa
hata na maji. Makatekista walisali kwa maombezi ya Sr. Irene basi maji ya
liyowekwa kwaajili ya ubatizo yalijaa na watu waliyatumia kwa kunywa na kuoga
kwa siku tatu.
Mwezi mmoja kabla ya kifo chake, Irene alienda
kwenye mafungo ya Kiroho, huko alimsikia Bwana Yesu akimwambia " Dhambi
zinanisulubu sana, yani ni heri maelfu wafe kuliko mtu mmoja kutenda
dhambi"
Sr. Irene alipokaribia kufa wanawake walioenda
kumuona walilia sana lakini yeye aliwaambia kwamba msilie mimi nakwenda
mbinguni. Alikufa akiyataja majina ya Yesu, Maria na Yosefu.
Historia hii fupi ya Sr. Irene imetafsiriwa kutoka : http://www.irenestefani.altervista.org/inglese/biografia_en.html
na http://mobile.nation.co.ke/news/Pope-puts-nun-who-worked-in-Nyeri-on-path-to-becoming-saint/-/1950946/2587262/-/format/xhtml/-/7kjtcq/-/index.html
Katika upendo wa Kristu,
Vincenzia- Marie!